BONDIA STANLEY MABESI 'NINJA' AMFAGILIA KOCHA SUPER D
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa katika picha na pamoja na bondia wa zamani Stanley Mabesi 'Ninja' wa pili kushoto ambaye kwa sasa anaishi nchini Holland mji wa Amsterdam wengine ni mashabiki wa mchezo wa masumbwi Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa pamoja na bondia wa zamani Stanley Mabesi 'Ninja' ambaye kwa sasa anaishi nchini Holland mji wa Amsterdam Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
BONDIA
wa siku nyingi Stanley Mabesi 'Ninja' aliekuwa akizipiga kuanzia mwana
1985 na kumalizia mpambano wake wa mwisho mwaka 2001 na kujijengea
heshima kubwa nchini juu ya mchezo wa masumbwi amempongeza kocha wa
kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
alipokuja hivi karibuni akitokea nchini Holland anapoishi kwa sasa.
Mabesi
alimpongeza Super D kwa kuwainua vijana mbalimbali katika mchezo wa
masumbwi, mojawapo ni kuwapa vifaa vya mchezo huo bure au hata
kuwapatia kwa gharama nafuu zaidi vifaa hivyo na kubuni njia moja wapo
na rahisi kwa kuwandalia DVD zenye mafunzo ya mchezo huo huku
akichanganya na mabondia mbalimbali wa nje wanaotamba Duniani.
Mabesi ambaye alitamba sana akiwa anacheza na Somwe Patauli,Felix Joseph,Emmanuel Kimaro,Charles Libondo.Eliud Morgan,Iraq Hudu,Deo Wanana,Rashid Matumla,George Sabuni,Maneno Oswald,Ramadhan Miyeyusho
mapambano hayo aliyocheza kwa nyakati tofauti ambayo yalikuwa ya kusisimua zaidi katika kipindi chake wakati anacheza vizuri sana mchezo uho wa masumbwi mchezo ambao una mashabiki wengi ila mpaka sasa umekosa wafadhili wanaojitokea kudhamini ambapo ni tofauti na nchi za wenzetu

No comments:
Post a Comment